RAS MHINTE ASISITIZA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WANANCHI.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Abdul Rajabu Mhinte Leo tarehe 19 Agosti 2025 amefanya kikao Cha Robo ya Nne ya Mwaka 2024/2025 na Sekretarieti ya Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri na Watendaji wa Taasisi za Umma katika ukumbi wa Karimjee 


Katika kikao hicho RAS Mhinte alisisitiza suala la utoaji wa huduma Bora kwa wananchi jambo ambalo ni matamanio na mategemeo yao . "Nchi imekua kiuchumi kwa sasa na maendeleo mengi yamepatikana kwa sababu ya uwajibika unaofanyika na kupelekea   jamii ya wana-Dar es Salaam kupata huduma Bora" *Alisisitiza RAS Mhinte*


Hata hivyo, Katibu Tawala alitaka uwepo wa Mawasiliano kati ya Taasisi Moja na nyingine  ili kuleta ufanisi mzuri wa utekelezaji wa miradi mbalimbali  inayoendelea katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuepuka matatizo au  changamoto zozote zinazoweza kujitokeza


Vile vile RAS Mhinte alisisitiza kero za wananchi kusikilizwa na kutatuliwa mara Moja. Wananchi wanapaswa kusikilizwa na kuhudumiwa kwa lugha nzur ili watoke wameridhika na huduma walizozipata


Hata hivyo, Katibu Tawala ameongeza kuwa Hamasa ya wananchi kujiandikisha kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025 inapaswa kuendelea kwani huu ni mwaka wa uchaguzi, kwa namna walivyojiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ndivyo hivyo wanapaswa kwenda kupiga kura


Ikumbukwe kuwa katika kikao Cha Robo ya Nne ya Mwaka 2024/2025 Watendaji wa Taasisi za Umma za Serikali waliwasilisha taarifa zao za mwaka wa fedha uliyoisha.



Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.