Afungwa Miaka 30 Jela kwa Kumbaka Mwanafunzi.


Morogoro

Mkulima, Deus Thadei Kupe (27), mkazi wa Kijiji cha Munga, Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa miaka 16 wa kidato cha kwanza na kumsababishia ujauzito.


Taarifa zinaeleza kuwa ujauzito huo uligundulika Agosti 19, 2025 katika Kituo cha Afya Mtimbira, baada ya vipimo kuonyesha kuwa mwanafunzi huyo alikuwa na ujauzito wa miezi sita.


Jeshi la Polisi lilifanya uchunguzi uliofanikisha kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, ambaye alipandishwa kizimbani na kutiwa hatiani baada ya ushahidi kuthibitisha bila shaka kosa hilo.


Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Alex Mkama alisema jeshi hilo halitasita kuwachukulia hatua kali watu wote watakaowarubuni au kuwanajisi watoto na wanafunzi.


Vitendo vya aina hii vinaharibu maisha na ndoto za watoto wetu. Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayejaribu kufanya ukatili wa namna hii,”alisema.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.