KAMANDA MULIRO AKABIDHI BENDERA KWA ASKARI WA KIKE WANAOKWENDA MAFUNZONI SCOTLAND.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Jumanne Muliro amewakabidhi bendera ya Taifa askari wa kike kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura wanaokwenda katika mafunzo ya Shirikisho la askari wa kike duniani (IAWP) nchini Scotland.



Kamanda Muliro amesema kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anathamini mchango wa shirikisho hilo ambalo limesaidia sana kuleta chachu ya mabadiliko ya kiutendaji ndani ya Jeshi la Polisi tangu waanze kushiriki mafunzo hayo katika maeneo tofauti tofauti duniani.



Aidha, amesisitiza kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi amewataka maafisa na askari hao wanaokwenda nchini Scotland kuwa na nidhamu muda wote wa mafunzo kama ilivyo kauli mbiu ya Jeshi la Polisi Tanzania, nidhamu haki weledi na uadilifu.



Sambamba na hilo amewakumbusha kutumia vyema mafunzo hayo kujenga mtandao wa mawasiliano ambao utaliunganisha Jeshi la Polisi Tanzania na mataifa mengine duniani katika kupambana na uhalifu na kubadilishana

uzoefu katika utendaji wa kazi za Polisi.



SACP Muliro amebainisha kuwa masomo ambayo yanakwenda kufundishwa ni Pamoja na Mkakati bunifu wa ulinzi kwa raia ili kuimarisha uaminifu kati ya vyombo vya sheria na jamii, kutumia sayansi data kuchunguza na kutabiri uhalifu, kupambana na ugaidi, uchunguzi wa kesi, biashara haramu ya binadamu na masomo mengine ambayo ni ya kimkakati katika kuzuia na uhalifu. 


Vilevile amewataka kutumia fursa hiyo kutangaza uzuri wa Tanzania na vivutio vilivyopo nchini.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.