MWENGE WA UHURU KATAVI 2025: RC MRINDOKO ATOA WITO WA UMOJA NA USHIRIKI MKUBWA KWA WANANCHI.


Katavi,

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko amesema maandalizi ya mapokezi na mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025 yamekamilika, huku akitoa wito kwa wananchi wote kushiriki kikamilifu katika tukio hilo muhimu la kitaifa.


Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 20

Septemba 2025, RC Mrindoko amesema kuwa Katavi itapokea Mwenge wa Uhuru tarehe 23 Septemba 2025 ukitokea mkoani Kigoma. Amefafanua kuwa mapokezi

yatafanyika katika kijiji cha lfumbula, Kata ya Mishamo, Tarafa ya Kabungu, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.



"Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa umbali wa

takribani kilomita 769 na utatembelea miradi 46 yenye thamani ya shilingi bilioni 10.25. Kati ya miradi hiyo, miradi 9 itawekewa mawe ya msingi, 25 itazinduliwa, 3 itafunguliwa,

8 itatembelewa na mradi mmoja utahusu ugawaji wa majiko

ya gesi," amesema Mkuu wa Mkoa.



Ameeleza kuwa Mwenge utakimbizwa kwa siku tano katika

halmashauri zote za mkoa, tarehe 23 Septemba 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, tarehe 24 Septemba

2025 Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, tarehe 25 Septemba 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, tarehe

26 Septemba 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, na tarehe 27 Septemba 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.



Amebainisha kuwa baada ya mbio hizo, tarehe 28 Septemba

2025 Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa kwa Mkoa wa Rukwa ili kuendelea na mbio zake kitaifa.

Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.