NLD YAHITIMISHA AWAMU YA KAMPENI KANDA YA KASKAZINI, YAJIPANGA KUELEKEA KANDA YA ZIWA.


Chama cha National League for Democracy (NLD) kimehitimisha rasmi awamu ya kampeni katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ikiwemo Tanga, Babati na Arusha, baada ya kufanya zaidi ya mikutano 45 kwa mfumo wa kijiji kwa kijiji na kata kwa kata.


Kampeni hizo zimekuwa za aina yake, zikifanyika kwa mtindo wa mobile kampeni, ambapo Mgombea Urais wa NLD, Mhe. Doyo Hassan Doyo, amekuwa akiwafuata wananchi moja kwa moja walipo, huku timu ya kampeni ikiendeleza mkakati wa nyumba kwa nyumba mara baada ya mgombea kuhamia wilaya nyingine.


Katika ziara hiyo, Mhe. Doyo alifika hadi maeneo ya pembezoni kama Jasini, Mkinga, Msomela, Handeni na Mlalo (Lushoto) — tofauti na wagombea wengine waliobaki zaidi mijini. Hatua hiyo imewavutia wananchi wengi, ambao wamesema wanajisikia kuthaminiwa na kuguswa moja kwa moja na mgombea wao.


Kwa mujibu wa tathmini ya chama, mkakati huu wa kampeni shirikishi umeimarisha uelewa wa wananchi kuhusu sera na ilani ya NLD, na kuonesha dhahiri kwamba chama kinajali kila Mtanzania bila kujali umbali wa eneo analoishi.


Baada ya mafanikio ya Kaskazini, sasa macho yote ya NLD yameelekezwa Kanda ya Ziwa  ikiwemo mikoa ya Mara, Mwanza, Geita, Bukoba na maeneo mengine ambapo mtindo wa mobile kampeni utaendelea kwa lengo la kusikiliza changamoto za wananchi moja kwa moja na kuzitafutia majibu kupitia ilani ya chama


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.