RC CHALAMILA ATOA SALAAM ZA POLE KUFUATIA VIFO 4 VYA MASISTA WA KANISA KATORIKI.


Dar es salaam,

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mhe Albert Chalamila leo Septemba 19, 2025 ameungana na waombolezaji katika Misa Takatifu ya Mazishi ya Masista wa shirika la Wakarmeli Wamisionari wa mtakatifu Teresia wa Mtoto   Yesu Boko Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.


Akitoa Salaam za Pole wakati wa Misa Takatifu ya Mazishi, RC Chalamila amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia anatoa pole kwa shirika na kanisa Katoriki kwa ujumla kufuatia vifo hivyo ambavyo vilitokana na ajali ya gari.


Pia Mkuu wa Mkoa ametoa pole na rambirambi ya shilingi milioni 10 pamoja na kuchangia milioni 10 nyingine kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kanisa la Parokia hiyo ya Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu.


 "Miili hii ya Masista ni pengo kubwa kwa Kanisa Katoriki na Shirika la Wakarmeli  Wamisionari wa Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu, Tuyapokee yote katika Kristo kama Biblia ilivyosema" Alisema RC Chalamila 


Ifahamike kuwa Masista hao 4  ambao ni Sr M. Lilian G Kapongo, Sr. M.Nerina De Simone, Sr. M. Damaris Matheka, Sr Stellamaris Muthini walifikwa na umauti Septemba 15,2025 kutokana na ajali ya gari lililogongana na gari kubwa Mkoani Mwanza.




Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.