Samia Aahidi Kuimarisha Kilimo cha Chikichi Kigoma.
Kigoma
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuimarisha kilimo cha chikichi mkoani Kigoma endapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akihutubia wananchi wa Kigoma Mjini leo Jumapili, Septemba 14, 2025, Samia alisema Serikali yake itatoa ruzuku ya pembejeo, mbegu na mbolea ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo, hatua itakayowavutia wawekezaji kuanzisha viwanda vya kukamua mafuta ya kula mkoani humo.
Aidha, aliahidi kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa ajili ya kuendesha viwanda, pamoja na kutekeleza mpango wa kuanzisha kongani za viwanda kila wilaya.
Akigusia madai ya fidia kwa wananchi waliopisha miradi ya maendeleo, Samia alisema Serikali ya CCM haitamdhulumu mwananchi, na kwamba uhakiki wa thamani ya ardhi unaendelea ili walipwe stahiki zao kwa wakati.

Comments
Post a Comment