Wateja wa HaloPesa Kunufaika na Milioni 2 Kupitia Kampeni ya “Tamba na Bonasi”

 


Dar es salaam,

Wateja wa HaloPesa sasa wanapata nafasi ya kujishindia hadi Shilingi Milioni 2 kila siku, wiki na mwezi kupitia kampeni mpya iitwayo “Tamba na Bonasi”. 


Kampeni hiyo, ambayo imezinduliwa leo September 19,2025 jijini Dar es Salaam, itadumu kwa miezi mitatu na ni sehemu ya mkakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya Halotel.


Kupitia kampeni hiyo, wateja wanaweza kushiriki kwa kufanya miamala ya kawaida kama kutuma na kupokea pesa, kutoa fedha, kulipia bili, kununua bidhaa na umeme wa LUKU huku huduma za kutuma pesa kutoka HaloPesa kwenda HaloPesa pamoja na ununuzi wa LUKU ni bure.



Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Idara ya Biashara wa HaloPesa, Bi. Happy Mzena, alisema:


“Kila muamala sasa ni fursa ya ushindi. Mr. Bonasi anawakilisha msisimko huu mpya kwa wateja wetu.”alisema bi Mzena




Kwa upande wake, Afisa Masoko, Bi. Aidat Lwiza, alisema:


“Tamba na Bonasi’ ni kampeni ya kipekee inayoongeza thamani na mvuto katika huduma zetu za kifedha.”alisema


Aidat aliongeza kuwa washindi wote watajulishwa kupitia ujumbe rasmi wa HaloPesa au kupigiwa simu kutoka namba ya huduma kwa wateja 100, huku akiwataka wateja kuwa waangalifu dhidi ya namba zisizo rasmi.



HaloPesa imesema kampeni hiyo inalenga kuongeza msisimko wa matumizi ya huduma zake, huku ikibaki kinara katika kutoa huduma nafuu, salama na zenye thamani kwa wateja wake kote nchini.






Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.