Watoto Wawili Wafariki Dunia kwa Moto Tabora, Mmoja Ajeruhiwa.


Tabora

Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia na mwingine kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali ya moto iliyotokea Septemba 13, 2025 katika eneo la Ikindwa, Kata ya Mapambano, Manispaa ya Tabora.


Taarifa za polisi zinaeleza kuwa moto huo ulianza baada ya mmoja wa watoto kuchezea kiberiti ndani ya chumba walicholala na kuwasha godoro lililoshika moto na kuwateketeza.


Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao, aliwataja waliofariki kuwa ni Jefta Hilari (6) na Eliana Hilari (4).


Alisema mtoto aliyenusurika lakini akijeruhiwa ni Osnili Hilari (7), ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Jeshi ya Milambo kutokana na majeraha ya moto.


“Mmoja wa watoto alikuwa akichezea kiberiti chumbani. Njiti ya moto ilipoangukia godoro, moto ulianza kushika na kuenea haraka. Wakati huo watoto walikuwa ndani peke yao, mama yao akiwa ameenda kanisani,” alisema Kamanda Abwao.


Moto huo pia uliteketeza mali zote zilizokuwemo ndani ya chumba hicho.

Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.