AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KOSA LA KUBAKA.


Nanyumbu, Mtwara


Mahakama ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela Mohamed Dokie Wema (35), fundi ujenzi na mkazi wa Kijiji cha Likokona, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mhanga mwenye umri wa miaka 75, mkulima na mkazi wa kijiji hicho.


Mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo Mei 30, 2025 katika Kitongoji cha Cheleweni, Kijiji cha Likokona, Wilaya ya Nanyumbu, baada ya kumvizia mhanga usiku akiwa amelala na kuingia ndani ya nyumba yake kisha kumbaka kwa nguvu.


Baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani tarehe Juni 4, 2025, ambapo alisomewa shtaka lake.


Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mhe. Asifiwe Jembe, na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Sajenti wa Polisi Deusdedith Ngobetse, baada ya upande wa mashtaka kujiridhisha pasi na shaka kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri, uliomuunganisha mtuhumiwa na kosa hilo.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.