HUDUMA YA INTANETI YAENDELEA KUKUA, WATUMIAJI WAFIKIA MILIONI 56.3


Huduma ya intaneti nchini imeendelea kukua kwa kasi, ambapo idadi ya watumiaji imeongezeka kutoka milioni 54.1 mwezi Juni 2025 hadi kufikia milioni 56.3 mwezi Septemba 2025. Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 4.1 katika kipindi cha miezi mitatu.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Takwimu zaSekta ya Mawasiliano ya robo mwaka inayoishia Septemba 2025, ongezeko hilo linahusisha laini au waya ambazo zimetumia huduma ya intaneti angalau mara moja katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Takwimu hizo zinahusisha teknolojia mbalimbali kama FTTX, 2G (GPRS na EDGE), 3G, 4G, na 5G.


Ripoti imeeleza kuwa huduma ya intaneti kwa njia ya simu za mkononi ndiyo inayotumika zaidi nchini, ambapo inachangia asilimia 99 ya matumizi yote ya intaneti. Huduma zisizo za mkononi, kama za nyumbani na za ofisini, zinachangia asilimia ndogo zaidi ya soko.


Kuongezeka kwa matumizi ya intaneti kunachangiwa na uboreshaji wa huduma unaofanywa na watoa huduma pamoja na kuimarika kwa miundombinu ya mawasiliano nchini. Hatua hii imewezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma za mawasiliano zenye kasi na ubora.


Aidha, upanuzi wa huduma za 4G na 5G umechangia kuongeza kasi ya upatikanaji wa intaneti na kurahisisha mawasiliano, biashara mtandaoni, na huduma za kijamii na kiuchumi zinazotegemea teknolojia ya kidijitali.


Ripoti pia imeonesha kuwa ongezeko hili linaendana na juhudi za serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora, salama na nafuu za mawasiliano, ikiwemo intaneti.

Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.