IDARA YA UHAMIAJI GEITA YASHIRIKI KIKAMILIFU ZOEZI IA ROUTE MATCH LILILOFANYIKA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA.
Na. Mwandishi wetu Geita.
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Geita ikiwa miongozni mwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini imeshiriki kikamillifu katika zoezi la Route Match lililoandaliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa ngazi ya mkoa.
Matembezi hayo yalianzia katika viwanja vya Kalangalala na kuelekea (Round about) ya Geita na kurudi viwanja wa kalangalala kwa mazoezi ya viungo vya mwili.
Mazoezi hayo yalihudhuriwa na Maafisa na Askari, kutoka Jeshi la Polisi, Jeshi La Magereza, Idara ya. Uhamiaji , Jeshi la Zimamoto na Uokoji, pamoja na Jeshi la Akiba.
Lengo la Mazoezi haya ya ukakamamavu ni ni kuleta ushirikiano baini ya vyombo vya ulinzi na usalama mkoani na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za dharura.
Mazoezi haya ya pamoja yatafanyika kila ljumaa, Yakilenga kuongeza ukakamavu na utayari. Hii itachangia kuboresha. ufanisi wa vyombo wa vyombo vya usalama na kuimarisha hali ya usalama katika jamii.




Comments
Post a Comment