JWTZ yatoa onyo kuhusu propaganda za kisiasa mitandaoni Kuhusu Jeshi hilo.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa tahadhari kwa umma wa Watanzania juu ya maudhui yanayosambazwa katika mitandao ya kijamii yenye lengo la kulihusisha Jeshi katika masuala ya kisiasa.
Katika taarifa iliyotolewa leo Oktoba 4, 2025, na kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Kanali Bernard Masala Mlunga, Jeshi hilo limesema kumekuwa na baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kueneza hoja zinazoashiria ushawishi wa kisiasa, huku wengine wakijinasibisha na Jeshi bila ridhaa.
“Baadhi ya hoja hizo zinatolewa na watu waliopo katika mazingira ya kijeshi, kujinasibisha na Jeshi, au waliowahi kuachishwa kwa mienendo mibaya na tabia zisizoendana na maadili ya kijeshi,” imesema taarifa hiyo.
JWTZ limeeleza kuwa linaendelea kutekeleza majukumu yake kwa uaminifu, utiifu na uhodari kwa mujibu wa kiapo chake, na kwamba halitashiriki katika harakati za kisiasa wala uanaharakati.
Jeshi hilo pia limewataka Watanzania kuendelea kuwa na imani nalo, kwani linadumu katika misingi ya kulinda taifa na wananchi wake bila upendeleo wa

Comments
Post a Comment