Kongamano la Wanavyuo Lafana, TAHLISO Yashukuru Washiriki.

 


Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO) imeishukuru jamii ya wanavyuo na wadau wa elimu kwa ushiriki wao katika Kongamano la Wanavyuo lililofanyika jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Ubungo Plaza, likiwa na dhamira ya kuwajengea vijana uelewa kuhusu nafasi yao katika mustakabali wa taifa.


Rais wa TAHLISO, Ndg. Geofrey Kiliba, alisema kongamano hilo limekuwa jukwaa muhimu la majadiliano kuhusu mchango wa vijana na wanavyuo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, likilenga kuhamasisha uzalendo, uelewa na ushiriki chanya wa vijana katika mchakato wa kidemokrasia nchini.


“Hakika tumejifunza mengi, na sasa tuko tayari kuyaishi kwa vitendo,” alisema Kiliba akisisitiza kuwa mafunzo, hoja na mijadala iliyojitokeza katika kongamano hilo itakuwa chachu ya mabadiliko na dira mpya kwa wanavyuo kote nchini.


Aidha, TAHLISO imepongeza ushiriki wa vyuo mbalimbali, viongozi wa serikali na wadau wa elimu waliotoa mchango wao mkubwa katika kufanikisha tukio hilo lililohusisha mafunzo, mijadala na uzoefu kutoka kwa wataalamu wa nyanja mbalimbali.


Jumuiya hiyo imesisitiza kuwa itaendelea kuratibu mijadala ya kitaaluma na makongamano kama hayo katika vyuo vikuu nchini ili kuendeleza mijadala yenye kujenga fikra na kuchochea ushiriki wa vijana katika maendeleo ya taifa.




Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.