Polepole aibua taharuki mitandaoni, Jeshi la Polisi lasema ukweli kuhusu madai ya kutekwa.



Jeshi la Polisi Tanzania limetoa taarifa rasmi likieleza kuwa bado linamsubiri mwanasiasa Humphrey Polepole kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) jijini Dodoma, ili kutoa maelezo kuhusu tuhuma mbalimbali alizotoa kupitia mitandao ya kijamii.


Katika taarifa iliyotolewa leo, Oktoba 6, 2025, na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, imeelezwa kuwa Polepole alitumiwa barua ya wito kisheria, lakini hadi sasa hajatekeleza maelekezo hayo kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.


“Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa bado linaendelea kumsubiri Ndg. Humphrey Polepole aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili atoe maelezo kuhusiana na tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia mitandao ya kijamii,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.


Aidha, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa limebaini kuwepo kwa taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kwamba Polepole ametekwa, na tayari limeanza kufanyia kazi taarifa hizo ili kubaini ukweli wake.


“Jeshi la Polisi limeona taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na ndugu zake kuwa ametekwa; tayari tumeanza kufanyia kazi taarifa husika ili kupata ukweli wake,” limeongeza jeshi hilo.


Taarifa hiyo imetolewa baada ya kuzuka kwa mijadala mikali mitandaoni kuhusu madai ya kutekwa kwa Polepole, hali iliyosababisha taharuki miongoni mwa wananchi na wafuasi wa vyama vya siasa.

Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.