SEGEREA YAITIKA KWA DK. SAMIA BONNAH KAMOLI.


MAELFU ya vijana, wadau wa michezo na viongozi wamejitokeza  kushiriki mbio za Jogging na Tamasha  la IJA Festival Season -1, lenye lengo la kuhamasisha wananchi kuchagua Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Familia Suluhu y na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Ladiaus  Kamoli.


Tamasha hilo limeongozww na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) , Mary Chatanda ambaye amewataka  vijana hususan wanamichezo kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 mwaka huu kumpigia kura Rais  Dk. Samia, ambaye ni mdau mkubwa wa michezo.


Chatanda , amesema  Ilani ya CCM ineeleza wazi  kuhusu kuboresha  sekta ya michezo hususan, viwanja  vya  michezo ili michezo  iwe ajira rasmi.


“CCM imeteua mgombea mzuri  wa urais Dk. Samia, ambaye naye anapenda michezo. Oktoba 29 kila mmoja  aende kupiga  kwani kura ni  haki yako ya msingi kuchagua kiongozi  wako kwa maendeleo,”amesema Chatanda.


Aidha amewataka vijana kuto kutishwa na uzushi wa Oktoba 29 kuwepo kwa maandamano.


“Msiogope, watu wanaosema kuna maandamano. Kwa ni nani anaye watisha vijana. Anaweza  kuwatishia nyau?Uchaguzi upo  na hawaitaiweza  serikali ya CCM” ameeleza.


Ameongeza  Rais Dk. Samia ndiye amiri jeshi mkuu  hivyo hakuna  atakaye furukuta kuingia barabarani.


 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Nasra Mohammed, aliwataka vijana wa mkoa huo kujitokeza kumpa kura za heshima Rais Dk. Samia.


Naye Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah, amewataka vijana hususan wana michezo kuhakikisha Oktoba 29 wanampigia kura Dk. Samia, yeye na  madiwani wote wa CCM katika Jimbo hilo.


Bonnah ameushukuru Umoja wa Vilabu vya Jogging Wilaya ya Ilala Kwa kuandaa tamasha hilo la aina yake lililopambwa pia na  burudani kutoka  kwa  nyota wa muziki  nchini.




Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.