SHULE YA SEKONDARI JUHUDI WAJIVUNIA MAFANIKIO MIAKA MITATU WAFAULU KWA ASILIMIA 100.


SHULE ya Sekondari Juhudi iliyopo wilayani Ilala mkoa Dar es Salaam inajivunia mafanikio makubwa katika ufaulu katika kipindi cha miaka mitatu  shule hiyo inafaulu umepanda kwa asilimia 100.


Akizungumza katika mahafali ya 21 ya shule ya Sekondari Juhudi Mkuu wa shule hiyo Happynes Pallangyo, amesema   katika kipindi cha miaka mitatu  takwimu za kitaaluma matokeo ya mtihani ya Taifa kidato cha nne NECTA kuanzia mwaka 2022  waliofanya mtihani 469 Ufaulu asilimia 84 mwaka 2023 waliofanya mtihani 440 Ufaulu asilimia 98 na mwaka 2024 569 waliofaulu asilimia 98.



"Shule yetu Sekondari ya Juhudi wahitimu wa kidato cha nne mwaka huu 2025 wanafunzi 746 wakiwemo wavulana 395 na wasichana 351 wote wameandaliwa vizuri watafanya vizuri katika mitihani yao ya Taifa wanatarajia kushika alama za juu kutokana na kuandaliwa vizuri katika mitihani mbalimbaliya majaribio" alisema Pallangyo. 


Akizungumzia historia ya shule amesema shule ipo kata ya Gongolamboto ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es salaam ambapo shule imejengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kipindi hicho .


Aidha amesema shule ya sekondari ya Juhudi ilizinduliwa  mwaka 2002 na Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Yusuph Makamba ikiwa na vyumba vinne vya madarasa na wanafunzi 90  na jengo moja la Utawala kwa sasa shule maendeleo kitaaluma imepandishwa hadhi na kuanzishwa kidato  cha tano .


"Shule yetu ya Sekondari Juhudi kuaanzia mwaka 2016 baada kupandishwa hadhi mpaka kufikia kidato cha tano kuanzia Julai 2016 inafundisha katika mchepuo ya HGL,HGE,HGK,HKL  na baadae itaongezeka ECsM.


Mwalimu Happynes Pallangyo amesema  kwa hatua ambayo shule hiyo  imefikia kwa kutambua mchango mkubwa uliofanywa na viongozi waliotangalia wakiongozwa na mkuu wa mkoa Dar es Salaam Yusuph Makamba na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Jiji la Dar es Salaam  pamoja na wadau wa sekta ya elimu.


Kwa upande wake mgeni rasmi Rais wa Tume ya Uhamasishaji Viongozi Wanawake wa harakati wa Umoja wa Shirikisho la Afrika Diaspora Emma Nyerere aliwataka wanafunzi wa Juhudi Sekondari huko waendako wakawe mabalozi wazuri kwa kuitangaza shule hiyo na kuwa na nidhamu na kufuata maadili mema. 





Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.