Takwimu Zinaonesha Saratani Zaendelea Kuongezeka, Wataalamu Watoa Wito kwa Jamii.


Na Fidea Masunga,Dar es salaam.


Takwimu za kitabibu zinaonyesha kuwa saratani ya shingo ya kizazi inaongoza miongoni mwa wanawake nchini, ikichangia karibu asilimia 30 ya wagonjwa wote, ikifuatiwa na saratani ya matiti kwa asilimia 15.


 Huku kwa wanaume, saratani ya tezi dume ndiyo inayoongoza, ikifuatiwa na saratani ya koo na saratani ya utumbo mpana (colorectal cancer), ambayo imepanda kwa kasi na sasa inashika nafasi ya tatu kitaifa.


Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la kimataifa la sarataniRais wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Saratani Tanzania, Dkt. Jerry Ndumbaro, aliwatoa hofu wananchi kwa kusema saratani zinaweza kutibika iwapo zitagundulika mapema.


“Changamoto kubwa ni kwamba wagonjwa wengi hufika hospitalini wakiwa katika hatua za mwisho. Saratani ikigunduliwa mapema, tiba yake huwa na mafanikio makubwa zaidi,” alisema Dkt. Ndumbaro.


Kwa upande wake, Dkt. Magreth Moshi, Daktari Bingwa wa Saratani hapa nchini, pamoja na Dkt. Isack Thomas, bingwa wa saratani kutoka Kenya, wamesema elimu kwa jamii, uchunguzi wa mapema, na mshikamano wa kikanda ni silaha muhimu za kupambana na ugonjwa huu.


“Tukianza elimu mapema mashuleni na vijijini, tutajenga kizazi kinachojua namna ya kujikinga na kuthamini uchunguzi wa afya mara kwa mara,” alisema Dkt. Moshi.


“Afrika Mashariki inakabiliwa na changamoto zinazofanana. Tukishirikiana katika tafiti na rasilimali, tutaokoa maisha ya maelfu ya wananchi wetu,” alisema Dkt.Isack


Hata hivyo wataalam wanasema ili kuepukana na ugonjwa wa saratani, jamii inapaswa kuchukua tahadhari kwa kubadili mtindo wa maisha, hasa kwa kula vyakula vyenye lishe bora na kufanya mazoezi mara kwa mara.







Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.