TMA yawatunuku waandishi wa habari tuzo za hali ya hewa 2025.
Waandishi wa habari nane wameibuka washindi katika Tuzo za Uandishi wa Habari za Hali ya Hewa kwa mwaka 2025 zilizotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Hafla hiyo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam, ililenga kutambua mchango wa wanahabari katika kuelimisha jamii kuhusu mabadiliko ya tabianchi na umuhimu wa kutumia taarifa sahihi za hali ya hewa.
Tuzo hizo pia zimelenga kutoa motisha kwa wanahabari kuendelea kuandika habari sahihi na za kuaminika zinazolenga kuelimisha na kuwalinda wananchi dhidi ya maafa kwa maendeleo ya uchumi wa nchi.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Jaji Mshibe Ali Bakari, Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, aliwataka wanahabari waliopata tuzo kutobweteka na kuendelea kuandika habari za za kuielimisha jamii kuhusu masuala ya hali ya hewa kwa uhakika,usahihi na kwa weledi.
“Endeleeni kuandika habari za hali ya hewa kwa maslahi ya kujenga Tanzania. Msibweteke, tunzeni tuzo hizi kama alama ya jitihada yenu,” alisema Jaji Bakari.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a, alisema mamlaka hiyo itaendelea kutoa motisha na mafunzo kwa wanahabari ili kuboresha utoaji wa taarifa sahihi kwa umma.
Miongoni mwa washindi hao ni Penina Malundo, Lisungu Kambona, Jerome Risasi, na Mariam Shabani ,Juma Issihaka, Zaitun Mkwama,James Salvatory pamoja naAmour Khamis Ali akiwa miongoni mwa waliotunukiwa tuzo hiyo kutoka Zanzibar.
Hata hivyo hafla hiyo pia iliambatana na warsha ya wanahabari ambayo iliangazia utabiri wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka (Novemba 2025 hadi Aprili 2026).


Comments
Post a Comment