TOENI MAPENDEKEZO YENYE TIJA KUBORESHA USIMAMIZI WA MAAFA NCHINI.


Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu) Brigedia Jenerali Hosea Ndagala amefungua Kongamano la Wadau wa Usimamizi wa Maafa linalofanyika kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Athari za Maafa kwa mwaka 2025.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo leo 12 Oktoba 2025 jijini Mbeya, Brigedia Jenerali Ndagala amewataka washiriki kuja na mapendekezo yenye tija katika usimamizi wa maafa.


"Kongamano hili limekusudiwa kuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto, na kutoa mapendekezo ya kuboresha mifumo ya kitaifa ya usimamizi wa maafa."


Vilevile amewataka washiriki kutumia fursa hiyo kuimarisha ushirikiano na kubuni njia mpya za kuongeza ustahimilivu wa jamii zetu ili kupunguza athari za maafa na kulinda maisha na mali.


Brigedia Jenerali Ndagala ametumia jukwaa hilo kuwashukuru wadau wote wanaendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu katika juhudi za kujenga Taifa lenye ustahimilivu dhidi ya majanga.






Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.