UHAMIAJI CLUB YAPAMBA MOTO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI MKOA WA DODOMA.


Dodoma.


Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma mapema wiki hii ilitoa elimu ya kiuhamiaji kwa Klabu ya Uhamiaji katika shule ya sekondari Msalato.

Maafisa na Askari waliofika shuleni hapo waliweka mkazo katika mada ya Uraia hasa ikizingatiwa kipindi tulichonacho ni cha maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani.


Mkaguzi msaidizi wa uhamiaji Sara Tama amewafundisha wanafunzi mada ya uraia, hususani aina za uraia, vigezo na taratibu za kuomba uraia kuanzia ngazi ya Kata, Wilaya, Mkoa, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji hadi kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi.


Mkaguzi Msaidizi Tama alieleza pia mada ya vibali kwa raia wa kigeni na kwa upande wa wanafunzi aliwaelimisha taratibu za kuomba kibali cha uanafunzi( student pass) alisema kibali hicho hutolewa kwa raia wa kigeni wanao kuja nchini kwa sababu za kujiendeleza ki Elimu, hivyo amewataka wanafunzi wageni wote kufika Ofisi za Uhamiaji kupata huduma au ufafanuzi zaidi wanapohitaji huduma za ki Uhamiaji.


Konstebo wa Uhamiaji Samantha Maruka alisema kupitia kampeni ya mjue jirani yako inayoendelea nchi nzima imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani raia wengi wa kigeni wanapata elimu na hufika ofisi za Uhamiaji kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.


Mwanafunzi Magreth Peter ambaye yupo kidato cha tano katika shule hiyo alitoa shukrani kwa ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma kwa kutoa kipaumbele katika shule yao ya Msalato kuipa kipaumbele cha kuendesha klabu ya Uhamiaji, amesema wanafunzi wote wamefurahi na wamejiunga na klabu hiyo kwani inatusaidia kuongeza uelewa wa vitu mbalimbali kuhusu idara ya Uhamiaji na nchi kwa ujumla.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.