VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA RUKWA VYAENDELEA KUJIIMARISHA ZAIDI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limefanya mazoezi ya pamoja yenye lengo la kuimarisha afya na mshikamano.
Matembezi hayo yamefanyika tarehe 04 Oktoba, 2025, katika maeneo mbalimbali ya mji wa kuimarisha Sumbawanga. Mazoezi hayo yalilenga kuimarisha mshikamano na maandalizi ya pamoja katika kulinda usalama wa wananchi na mali zao.
Mazoezi hayo yaliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mheshimiwa Nyakia Ally Chilukile, ambaye alisisitiza umuhimu wa vyombo vya ulinzi kushirikiana kwa karibu katika kuhakikisha hali ya amani na usalama inaendelea kudumu mkoani Rukwa.
Mhe Chilukile alisema mshikaman huo ni nyenzo muhimu ya kujenga imani ya wananchi kwa Serikali na vyombo vya ulinzi.
Shughuli hizo za mazoezi zilihitimishwa katika viwanja vya Wizara ya Mambo ya Ndani mjini Sumbawanga.




Comments
Post a Comment