WAGOMBEA UBUNGE NA MAWAKALA WA KAWE, KINONDONI WAPEWA KIAPO.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


MSIMAMIZI Mkuu wa Uchaguzi wa Wilaya ya Kinondoni, Bi. Magreth Mangasa, ameongoza zoezi la kiapo kwa wagombea wa ubunge na mawakala wao kutoka vyama vyote vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa majimbo ya Kawe na Kinondoni.


Zoezi hilo limefanyika leo, Oktoba 21, 2025, katika ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, likiwa ni sehemu ya maandalizi rasmi kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.


Akizungumza wakati wa tukio hilo, Bi. Mangasa alisema kiapo hicho kimefanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 40(6) ya Uchaguzi ya mwaka 2025, inayowataka wagombea na mawakala kula kiapo siku saba kabla ya uchaguzi.


Alisema kiapo hicho kinawapa uhalali wa kuingia kwenye vituo vya kupigia kura, kushuhudia zoezi la kuhesabu kura na kujumlisha matokeo, sambamba na kuwabebesha wajibu wa kutunza siri na kuheshimu taratibu zote za uchaguzi.


“Ni muhimu kwa kila wakala kutambua wajibu wake wa kulinda siri za uchaguzi, kuzingatia sheria na kuhakikisha utulivu katika vituo vyote vya kupigia kura,” alisema Bi. Mangasa.


Aliongeza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuhakikisha uwazi, uadilifu na usimamizi bora wa mchakato wa uchaguzi katika majimbo hayo mawili.






Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.