WATUMISHI TFS KANDA YA MASHARIKI WATAKIWA KUWAJIBIKA KIKAMILIFU

 


Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Mashariki wametakiwa kuwajibika kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa kuzingatia weredi, uadilifu na uwajibikaji wa hali ya juu.


Maelekezo hayo yametolewa leo na Kamanda wa Kanda ya mashiriki  PCO Mathew Ntilicha kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo, wakati wa kikao cha watumishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikoko, Makao Makuu ya Kanda, eneo la Loliondo, Wilaya ya Kibaha.


Akizungumzia changamoto za kiutendaji miongoni mwa watumishi, PCO. Ntilicha alisema kuwa ni muhimu kwa kila mtumishi kuwa na mpango kazi wa wiki, mwezi na mwaka unaoendana na majukumu yake ya kitaasisi kama alivyo pangiwa. Alibainisha kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na uwajibikaji wa pamoja.


Aidha, alisisitiza kuwa Ofisi ya TFS Kanda ya Mashariki itaendelea kushughulikia changamoto mbalimbali za kiutendaji ili kuhakikisha mazingira bora ya kazi yanakuwepo kwa watumishi wote, sambamba na matumizi sahihi ya teknolojia ya mifumo ya utoaji taarifa.



Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.