JESHI LA POLISI LATOA ONYO KALI DHIDI YA WATU WANAOTOA MATAMKO YA KUCHOCHEA CHUKI NA KUVURUGA AMANI.


Jeshi la Polisi nchini limesema linaendelea kufuatilia kwa ukaribu hali ya usalama na kuchukua hatua kwa ukiukwaji wowote wa sheria, huku likionya makundi na watu binafsi wanaotoa matamko ya kuchochea chuki na kuvuruga amani.


Jeshi la Polisi limeeleza kuwa kumekuwapo na makundi mbalimbali pamoja na watu binafsi ambao wamejitokeza na kutoa matamko yenye viashiria vya uvunjifu wa amani na kuchochea chuki miongoni mwa jamii, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.


Katika taarifa yake, Jeshi hilo limesema halitasita kuchukua hatua dhidi ya matamko yoyote yenye lugha laini au kali yanayoweza kusababisha uchochezi.


 Pia limesisitiza kuwa hatua zitachukuliwa kwa vitendo na kauli zote zenye lengo la kuchochea vurugu na kuyumbisha utulivu wa taifa.


Jeshi la Polisi limekumbusha kuwa katika kipindi hiki ambacho nchi inaendelea na juhudi za maridhiano na ujenzi wa umoja wa kitaifa, ni muhimu kulinda amani na utulivu ili uchumi na shughuli za kijamii ziendelee kukua. 


Pia Limeonya kuwa endapo vurugu zitatokea, athari zitamgusa kila mwananchi katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kiusalama.



Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.