MADEREVA MWENDOKASI MBAGALA WAPEWA MAFUNZO MAALUMU KUDHIBITI AJALI.


Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi Temeke, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Africanus Sulle, amefungua mafunzo maalumu ya siku mbili kwa madereva wa mabasi yaendayo kasi katika Barabara ya Kilwa, katika kituo kikuu cha mabasi hayo kilichopo Mbagala.


Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, SSP Sulle amewataka madereva hao kuzingatia mafunzo wanayopatiwa, ambayo yamelenga kuimarisha utii wa Sheria za Usalama Barabarani ili kudhibiti ajali zisizokuwa za lazima.


Kwa upande wake, Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama Barabarani Temeke, Mkaguzi wa Polisi Emmanuel Matei, amewahimiza madereva hao kuzingatia kanuni za udereva, hususan mbinu za Udereva wa Kujihami, ili kuepusha ajali na kuhakikisha usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara.


Aidha, Mkaguzi Matei ametoa wito kwa viongozi na madereva hao kushirikiana katika kutunza mabasi ya mwendokasi pamoja na miundombinu yake kwa ujumla, ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na huduma hiyo kwa muda mrefu.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.