MAKAMU WA RAIS NCHIMBI AMWAKILISHA RAIS SAMIA LUSAKA KATIKA UWEKAJI JIWE LA MSINGI WA RELI YA TAZARA.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewasili jijini Lusaka leo akitarajiwa kumwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la uzinduzi wa ukarabati mkubwa wa Reli ya TAZARA, itakayofanyika kesho, Novemba 20, 2025.


Makamu wa Rais alipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda na Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Dkt. Elijah Muchima, Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, pamoja na maafisa waandamizi wa pande zote mbili. Viongozi hao pia walipokelewa na vikundi vya ngoma vilivyopangwa kwa heshima yake.


Pamoja na viongozi wengine, Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Masanja, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Salum.




Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.