NIT YATOA MAFUNZO KWA WAHUDUMU WA MABASI YA MASAFA MAREFU NA MIJINI JIJINI TANGA.
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kupitia Idara ya Usalama katika Usafirishaji na Uhandisi wa Mazingira (TSEE) kwa kushirikiana na Muungano wa Wasafirishaji Jijini Tanga (MUWATA), kimetoa mafunzo maalum kwa wahudumu wa mabasi ya masafa marefu na ya mijini mkoani Tanga.
Mafunzo hayo, yaliyofanyika kuanzia tarehe 17 – 22 Novemba 2025, yalishirikisha jumla ya washiriki 34 ambao wametunukiwa vyeti baada ya kukamilisha mafunzo hayo.
Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Chuo, Mhadhiri kutoka Idara ya Usalama katika Usafirishaji na Uhandisi wa Mazingira, Dkt. Mary Makyao, aliwahimiza washiriki kutumia elimu na ujuzi walioupata ili kuboresha utendaji katika maeneo yao ya kazi.
Kwa upande wake, Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Tanga, Ndg. Shedrack Malale, amelishukuru Chuo kwa kuendesha mafunzo hayo kwa mara ya tatu jijini Tanga, akibainisha kuwa yatasaidia kuongeza ufanisi na ubora wa huduma za usafirishaji nchini.


Comments
Post a Comment