Polisi Wangingombe Watoa Elimu ya Usalama Barabarani, Wahimiza Madereva Kuheshimu Sheria.


Na Mwandishi Wetu, Njombe


Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limeendelea na kampeni zake za kutoa elimu kwa madereva na watumiaji wa barabara, likilenga kupunguza ajali na kulinda maisha ya wananchi.


 Hayo yameelezwa na Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Wangingombe, Mkaguzi Benedict Onesmo Mkuti, alipotoa elimu hiyo katika eneo la Igwachanya, mkoani Njombe.


Mkaguzi Mkuti aliwataka madereva kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani ili kupunguza ajali zisizo za lazima ambazo zimekuwa zikisababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali, akisisitiza kuwa lengo kuu la Jeshi la Polisi ni kuhakikisha abiria wanafika salama wanakoelekea.


Aidha, aliwahimiza abiria na wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa kuhusu madereva wanaokiuka sheria, ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wakati.


Elimu hiyo ni sehemu ya jitihada endelevu za Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha usalama barabarani unaimarika na kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.