TMA YATAHADHARISHA MVUA KUBWA KWENEYE MIKOA KADHAA TANZANIA .
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali mbaya ya hewa kuanzia Alhamisi, Novemba 20 hadi Jumapili, Novemba 23, 2025, kwa baadhi ya maeneo ya nyanda za juu kusini na magharibi mwa nchi.
Kwa siku ya Alhamisi, Novemba 20, 2025, angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Ruvuma na Njombe, ambapo athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji.
Ijumaa na Jumamosi, Novemba 21–22, 2025, mvua kubwa inatarajiwa kuendelea katika maeneo machache ya mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Morogoro, Singida, Dodoma, Kigoma, Katavi na Tabora. Athari zinazotarajiwa bado ni zilezile za makazi kuzungukwa na maji, huku TMA ikisisitiza wananchi kuchukua tahadhari na kuzingatia taarifa za utabiri.
Kwa siku ya Jumapili, Novemba 23, 2025, hakuna tahadhari yoyote iliyotolewa na TMA.
TMA imewahimiza wananchi, hasa wanaoishi maeneo hatarishi, kufuatilia taarifa rasmi na kuchukua tahadhari stahiki ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.


Comments
Post a Comment