Uteuzi: Rais Samia Awateua Wabunge Sita wa Bunge la Kumi na Tatu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewateua wabunge sita wa Bunge la Kumi na Tatu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba ya Nchi ya mwaka 1977.
Walioteuliwa ni Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, Bw. Abdullah Ali Mwinyi, Balozi Khamis Mussa Omar na Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka, imeeleza kuwa uteuzi huo unaanza mara moja.
Uteuzi huu unatarajiwa kuimarisha uwakilishi wa kitaalamu na uzoefu katika Bunge jipya la Kumi na Tatu, ambalo linaanza kikao chake cha kwanza Novemba 11, 2025, jijini Dodoma.


Comments
Post a Comment