WATAALAMU WA TIMU YA JICA KWA MRADI WA USALAMA BARABARANI WAFANYA ZIARA FUPI NDANI YA KITENGO CHA HUDUMA DHARURA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA AMANA.


Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana imepokea ugeni kutoka timu ya wataalam wa JICA walioko nchini kwa ajili ya mradi wa Usalama Barabarani. Katika ziara hiyo fupi, wataalam hao walitembelea kitengo cha huduma za dharura na kujionea namna huduma zinavyotolewa.


Wageni hao walipokelewa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Amana, Dkt. Bryceson Kiwelu, ambaye aliwakaribisha na kuwapa maelezo kuhusu maboresho mbalimbali yanayoendelea hospitalini hapo.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Fukushima daktari bingwa wa dharura kutoka Hospitali ya Saiseikai Kazon chini Japan alieleza kufurahishwa kwake na jinsi kitengo cha dharura cha Amana kilivyojipanga kutoa huduma kwa umakini, uharaka na weledi. 


Alisifu mifumo ya utoaji huduma,utayari wa watumishi, pamoja na maboresho yanayoendelea kufanywa ili kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi.


Ugeni huo umetoa fursa ya kubadilishana uzoefu kati ya wataalam wa afya wa Tanzania na Japan, huku JICA ikionesha utayari wa kuendelea kushirikiana na Amana katika maeneo yanayohusiana na usalama barabarani na huduma za dharura.


Aidha, Dkt. Kiwelu alishukuru kwa ziara hiyo na kusisitiza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuboresha huduma za dharura kwa kiwango cha kimataifa.



Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.