WATU WATANO WAFARIKI NA MMOJA KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA MAGARI MBUNYUNI, MONDULI, MKOANI ARUSHA.


Watu watano wafariki na mmoja kujeruhiwa katika ajali ya kugongana kwa gari mawili iliyotokea tarehe 23 Novemba 2025, saa 07:00 mchana, eneo la Mbuyuni, wilaya ya Monduli, mkoani Arusha. 


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,imesema  basi la abiria lenye namba za usajili T. 922 DZQ aina ya Yutong, likitokea Dodoma kuelekea Arusha, liligongana na gari ndogo la abiria lenye namba T. 705 DFP aina ya Mark X lililokuwa likitokea Arusha.

Waliofariki ni wanaume watatu na wanawake wawili, wote wakiwa abiria wa vyombo hivyo ambapo majeruhi mmoja, yupo Hospitali ya Jeshi Monduli akiendelea kupatiwa matibabu, huku miili ya marehemu ikiwa imehifadhiwa Kituo cha Afya Makuyuni kwa taratibu za kisheria.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ameeleza kwamba chanzo cha ajali bado kinachunguzwa na mamlaka husika ambapo uchunguzi unaendelea ili kubaini sababu halisi zilizosababisha tukio hilo na kuhakikisha hatua zinazofaa zinachukuliwa ili kuimarisha usalama barabarani.


Jeshi la Polisi limetoa wito kwa madereva na watumiaji wote wa vyombo vya moto kuchukua tahadhari, kufuata sheria, kanuni, na taratibu za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kusababisha vifo, majeruhi au uharibifu wa mali. 


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.