CCM HAITASITA KUWACHUKULIA HATUA WATUMISHI WA UMMA WABABAISHAJI - MWENEZI KENANI.

 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na MafunzoNdugu Kenani Kihongosi, amewataka watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao kwa weledi, kwa kutanguliza utu na muda, huku akisisitiza kuwa chama hakitasita kuwachukulia hatua wale watumishi ambao wanapuuza wajibu wao au kuwababaisha wananchi.


Akizungumza na viongozi wa chama na jumuiya za mkoa wa Dar es Salaam, Mwenezi Kenani alisema kuwa baadhi ya watumishi wa umma wamekuwa wakilalamika kuhusu ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali, jambo ambalo alisema ni dalili ya kutokutimia majukumu yao kikamilifu.


“Kuna baadhi ya watumishi wa umma wanasema chama kinawafatafata, waambieni tuna wajibu wa kuwafata kwani ilani inayotekelezwa ni yetu na tutawafata kila wakati kuhakikisha wanafanya kazi iliyokusudiwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,” alisema Mwenezi Kenani.


Alisisitiza kuwa kitendo cha kutotekeleza majukumu kwa ufanisi ni kukosea heshima serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inatokana na CCM na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Mwenezi Kenani alifafanua zaidi kuhusu ufuatiliaji wa miradi, akisema:


“Ikiletwa fedha ya kituo cha afya, basi chama kitakuja kukagua matumizi sahihi ya fedha hizo. Hatutaacha kufanya hivyo kwani watumishi wazembe ndiyi wenye kusababisha CCM ionekane haifanyi kazi.”


Kauli hiyo inafafanua dhamira ya CCM kushirikiana na watumishi wa umma kuhakikisha utekelezaji wa miradi unafanyika kwa uwazi, kwa manufaa ya wananchi na kwa kufuata ilani ya uchaguzi ya chama hicho.


Mwenezi Kenani ameongeza kuwa chama kina wajibu wa kuendelea kufuatilia utekelezaji wa ilani na miradi, ili kuhakikisha serikali inatekeleza ahadi zake kwa wananchi kwa uwazi, weledi, na uwajibikaji.

Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.