DAWA ZA ARV ZAPATIKANA KWA 100% – WAZIRI LUKUVI


Dar es Salaam. 


Serikali imesema upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya VVU (ARV) kufikia asilimia 100 katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini, hatua inayodhihirisha uimara wa mfumo wa tiba na mwitikio wa taifa katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI. 


Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (SBUU), Mhe. William Lukuvi, wakati wa kutoa Tamko la Serikali kuhusu Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani 2025 chini ya kaulimbiu: “Imarisha Mwitikio, Tokomeza UKIMWI.”


Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Waziri Lukuvi alieleza kuwa kiwango hicho cha upatikanaji kimetokana na maboresho makubwa ya kimfumo katika maeneo ya ununuzi, ugavi, na ufuatiliaji wa dawa. Hatua hizo zimehakikisha kila kituo cha afya kinapata ARV kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa, na hivyo kuwezesha watu wanaoishi na VVU kupata huduma bila usumbufu na bila gharama.


Akiwasilisha tathmini ya utekelezaji kwa mwaka 2025, Waziri Lukuvi alisema matumizi ya ARV yameendelea kuongezeka kutoka asilimia 98 mwaka 2024 hadi asilimia 98.5 mwaka 2025 ambapo dadi ya vituo vinavyotoa huduma za VVU/UKIMWI imefikia 8,203 kutoka 7,805, hatua inayodhihirisha kupanuka kwa upatikanaji wa huduma katika maeneo mbalimbali ya nchi. 


Vilevile, mashine za kupima wingi wa VVU (Viral Load) zimeongezeka na sasa zimefikia 177, ikijumuisha mashine 43 kubwa na 127 ndogo, jambo linaloimarisha uwezo wa kufanya uchunguzi wa uhakika na kuongeza usahihi wa ufuatiliaji wa tiba.


Waziri Lukuvi alisisitiza kuwa Serikali, kwa ushirikiano na wadau, itaendelea kuwekeza katika elimu kwa jamii, kuboresha miundombinu ya huduma, na kupunguza maambukizi mapya. 


Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kupima afya, kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya, na kutumia ARV kwa kufuata maelekezo, ili kufanikisha malengo ya kitaifa na kimataifa ya kutokomeza UKIMWI kama tishio la afya ya umma.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.