Popular posts from this blog
RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es alaam Mhe Albert Chalamila amewataka wenyeviti wa Serikali za mitaa pamoja na watendaji wa Kata Mitaa Mkoani humo kusimamia ulinzi na usalama kwenye ngazi ya mitaa na kata ili kuhakikisha Mkoa huo unakua Salama bila uwepo wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati wote. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na Wenyeviti, Watendaji wa Kata na mitaa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Diamomd Jubilee RC Chalamila amesema suala la ulinzi na usalama linapaswa kuanzia kwenye ngazi ya mitaa na kata hivyo amewataka viongozi hao wa mitaa kusimamia suala hilo kwani katika baadhi ya mitaa kumekua na matukio ya uvunjifu wa amani. RC Chalamila amewataka viongozi hao ngazi ya Mitaa na Kata kusaidia kutatua changamoto za wananchi na sio wao kuwa ni chanzo cha kuongeza changamoto kwa wananchi ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuwataka wenyeviti na watendaji kutambua kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo waendelee kuhimiza wananchi kuanzia ngazi ya mtaa kushiriki ucha...
MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.
Na Fidea Masunga,Dar es Salaam. Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuhakikisha wanawalea watoto katika misingi ya maadili, nidhamu na hofu ya Mungu ili kujenga kizazi chenye kuzingatia elimu, kuishi maisha ya wema na kuwa viongozi bora wa kesho. Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na mdau wa elimu Ramadhan Balle , ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya nane ya Shule ya Awali na Msingi Sai yaliyofanyika Chanika Kidugalo Dar es salaam. Akizungumza kwenye hafla hiyo, Balle alisema malezi bora ya watoto hayapaswi kuishia nyumbani pekee, bali yazingatie misingi ya kiroho kupitia maandiko ya dini kama Biblia na Qur’ani, kwani ndiyo msingi wa kujenga jamii yenye hofu ya Mungu na kuondokana na vitendo vya ukatili na maovu. “Watoto wakilelewa katika msingi wa dini, wanakua na mwelekeo bora, wanajengeka kiakili na kiroho na hivyo kuepuka kujiingiza katika tabia hatarishi. Hili ni jukumu lenu wazazi na walezi,” alisema Balle. Aidha, aliwataka wazazi kuwekeza zaid...




Comments
Post a Comment