KANISA LA MANM LAHITIMISHA MFUNGO WA SHUKRANI KWA KUTOA ZAWADI KWA YATIMA, WAJANE NA WENYE UHITAJI.


Dar es Salaam.


Kanisa la MANM lililopo Tabata Kisukuru,Dar es salaam limehitimisha rasmi mfungo wa siku 14 wa shukrani kwa kufanya ibada maalumu iliyohusisha zoezi la kutoa misaada kwa yatima, wajane, wazee na familia zenye uhitaji kutoka maeneo mbalimbali ya jirani.


Ibada hiyo ilihudhuriwa na waumini, viongozi wa mtaa, pamoja na walengwa wa misaada ambapo Akizungumza kabla ya kuanza kwa ugawaji wa misaada, mbeba Maono wa Kanisa la MANM Askofu Nabii Evans Sindano alisema:


“Neno bila matendo halitoshi. Tunapomaliza mfungo, Mungu anatukumbusha kuwa ushindi wa kweli ni kugusa maisha ya wengine.


Aliongeza kuwa;


“Kila zawadi tunayoitoa leo ni mbegu ya tumaini na upendo kwa walio katika mazingira magumu. Hii ni njia ya kueneza mshikamano katika jamii na kuhakikisha kuwa kila mmoja anahisi umuhimu wake katika maendeleo ya taifa letu.”


Viongozi wa mtaa waliokuwepo walilipongeza kanisa la MANM kwa kuendelea kuwa tegemeo la jamii huku mmoja wa wahitaji ambae ana ulemavu wa miguu Bw.Ismail Mwingira aliyepokea misaada alisema:


“Tumekuwa tunapitia changamoto nyingi, lakini leo tumepata faraja. Tunashukuru kwa kutukumbuka.”alisema Ismail.


Wajane waliopokea misaada pia walieleza shukrani zao akiwemo Bi.Costancia Lazaro alieleza kuwa;


“Kanisa la MANM limekuwa msaada wetu wa kweli. Zawadi hii imetugusa,imetufariji na kututia nguvu,” alisema mjane huyo.


 Misaada hiyo ilitolewa kwa yatima,wajane na wahitaji zaidi ya 50  ambapo walipewa zawadi za vyakula, mavazi, vifaa vya shule na mahitaji mengine ya msingi huku zoezi hilo likihitimishwa kwa kula chakula cha pamoja kama ishara ya mshikamano, furaha na shukrani baada ya mfungo. 


Tukio hilo pia limeonesha nafasi ya kanisa katika kuimarisha mshikamano wa kijamii, kushirikiana na viongozi wa mtaa na kuendeleza maendeleo ya jamii kwa ujumla.




Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.