MKUU WA WILAYA YA MTWARA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA KASI YA UPAKIAJI KOROSHO, AWAPONGEZA MAKANJIRO, MAXIMA, MTUWASA NA TANESCO.

 


Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya, ameendelea na ziara yake ya kikazi kukagua mwenendo wa shughuli za upakiaji wa korosho katika Bandari ya Mtwara.


Ziara hiyo ni kufuatia taarifa za awali zilizoonesha kupungua kwa kasi ya utendaji katika mchakato huo muhimu kwa msimu wa usafirishaji wa korosho.


Katika ziara hiyo, Mhe. Mwaipaya alitembelea maeneo ya kuhifadhi mizigo, maeneo ya maandalizi nje ya bandari, pamoja na maeneo ya upakiaji ndani ya bandari, ambako alipata fursa ya kujionea mwenendo wa kazi na kujadiliana na wasimamizi kuhusu changamoto na hatua zinazochukuliwa.


Aidha, DC Mwaipaya alizipongeza kampuni za Makanjiro na Maxima kwa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kasi inayotakiwa, akizitaja kama mfano unaopaswa kuigwa na wadau wengine katika mnyororo wa usafirishaji wa korosho.


Vilevile, alitoa pongezi kwa MTUWASA na TANESCO kwa kuhakikisha huduma muhimu za maji na umeme zinapatikana katika maeneo ya ndani na nje ya bandari, hali iliyosaidia kuongeza ufanisi na kurahisisha shughuli za upakiaji.

Akisisitiza zaidi, DC Mwaipaya aliwahimiza wawekezaji wengine kujitokeza, akifafanua kuwa serikali imeandaa maeneo maalumu kwa ajili ya shughuli za staffing, hivyo kutoa fursa za kuongezeka kwa nguvu kazi na ufanisi katika mnyororo mzima wa usafirishaji wa korosho.


“Maeneo yapo, mazingira ya uwekezaji ni rafiki. Tunakaribisha wawekezaji zaidi ili kuongeza kasi, kuboresha ufanisi na kupunguza msongamano katika msimu huu,” aliongeza.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.