MWIGULU: TUTAMUENZI KWA VITENDO MAREHEMU JENISTA.


WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itayaendeleza mambo yote mema yaliyofanywa na aliyekuwa mbunge wa Peramiho mkoani Ruvuma, Marehemu Jenista Mhagama ikiwemo kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za kidini.


Amesema marehemu Jenista alikuwa mpatanishi akiunganisha makundi mbalimbali yakiwemo ya wafanyakazi na Serikali ambapo hadi leo wanaushirikiano mkubwa, pia aliimarisha umoja na mshikamano kati ya Serikali na sekta binafsi na alifanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa.



"Marehemu Jenista amekuwa anaamini katika mafanikio na hiyo ndio iliyompa jina la kiraka kwa kuwa kila nafasi aliyopewa aliimudu kwa ukamilifu. Jenista amegusa maisha ya wengi, mimi nilikuwa nashirikiana naye katika masuala ya uongozi na alikuwa mmoja wa marafiki wa familia."



Ameitoa kauli hiyo leo Jumatatu, Desemba 15, 2025, wakati akiwasilisha salamu za Serikali aliposhiriki Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jenista Mhagama iliyofanyika katika kanisa Katoliki la Abasia ya Mtakatifu Benedicto, Peramiho.



Katika salamu hizo, Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, amemuagiza awahakikishie Watanzania wakiwemo Wana-Ruvuma kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao kama ilivyokuwa inafanya wakati wa uhai wa Jenista.



"Mheshimiwa Jenista alikuwa kiungo kati ya Wana-Ruvuma na Wana-Peramiho na alikuwa kiungo kati ya Kanisa na Serikali, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amenituma niwahakikishie wote kwamba Serikali itaendelea kuyaenzi mema yote aliyoyafanya enzi za uhai wake."



Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.