NAIBU WAZIRI KIHENZILE AFUNGUA MKUTANO WA 18 WA PAMOJA WA MAPITIO YA SEKTA YA USAFIRISHAJI.


Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile, Disemba 15, 2025 amefungua rasmi Mkutano wa 18 wa Pamoja wa Mapitio ya Sekta ya Usafirishaji unaofanyika katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.


Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mhe. Kihenzile alisema kaulimbiu ya mkutano huo isemayo "Integrated Transport System as a Foundation for Economic Transformation Toward Vision 2050" inaonesha nafasi ya sekta ya usafirishaji kama nguzo muhimu ya mabadiliko ya kiuchumi na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.


Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mfumo jumuishi wa usafirishaji unaounganisha barabara, reli, bandari, maji, usafiri wa anga pamoja na kukamilisha na kupanua miradi mikubwa ya miundombinu.


Upande wa meli amesema Serikali inaendelea na ukarabati wa meli zilizopo, ujenzi wa meli mpya na kiwanda cha kutengeneza meli hali itakayochochea muunganiko na ukuaji wa uchumi kikanda.


Vilevile, Mhe. Kihenzile amekipongeza chuo cha bahari kwa huduma bora inayotoa hususani katika kuwafundisha mabaharia na kuwajengea uwezo wa kitaalamu na kiufundi unaohitajika katika soko la ajila kitaifa na kimataifa.


Aidha Makamu Mkuu wa Chuo cha Bahari (Taalama) Prof. Wilfred Kileo alitoa maelezo mafupi kuhusu elimu na mafunzo yanayotolewa na Chuo pamoja na kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi kila mwaka.


Mkutano wa 18 wa pamoja wa mapitio ya sekta ya Uchukuzi utafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 15 mpaka 17 Desemba, 2025 ambapo unatarajiwa kutoa mapendekezo muhimu yatakayosaidia kuboresha Sera.






Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.