NAIBU WAZIRI LONDO ASISITIZA UMUHIMU WA KULINDA AMANI.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dennis Lazaro Londo, amesisitiza umuhimu wa kulinda na kuendeleza amani nchini akieleza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii.


Mhe. Londo ametoa kauli hiyo leo aliposhiriki katika ibada maalumu ya kumuwekea Wakfu na kumuingiza kazini Askofu Msaidizi wa Dayosisi ya Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt George Andrew Pindua mkoani Morogoro, Disemba 14, 2025.


Naibu Waziri Londo, amesema kuwa jamii ina wajibu wa kuishi kwa kuzingatia maadili ya imani kama dini zetu zinavyofundisha.


Aidha, amesisitiza kuwa binadamu wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu, hivyo wanapaswa kuishi katika misingi ya amani na upendo.





Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.