RAIS SAMIA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MBUNGE WA PERAMIHO, MHE. JENISTA MHAGAMA.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo ameongoza waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mhe. Jenista Joakim Mhagama. Ibada hiyo ilifanyika Kanisa la Mwenyeheri Maria-Theresa Ledochowska, Parokia ya Kiwanja cha Ndege, Dodoma.


Akizungumza kwenye ibada hiyo, Rais Dkt. Samia alieleza huzuni kubwa ya Taifa kufuatia kifo cha Marehemu, akimuelezea kama kiongozi jasiri, mwaminifu na mlezi wa viongozi wengi, aliyejitolea kwa moyo wote kwa maendeleo ya wananchi. Alisisitiza kwamba Marehemu alisimama imara kutetea haki, usawa na maendeleo ya wananchi.


Aidha, Rais alitambua mchango wa Marehemu katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Serikali na Chama cha Mapinduzi, sambamba na uwezo wake wa kubeba majukumu makubwa kwa weledi. Alitoa wito kwa viongozi kuiga mfano wake wa maadili na uwajibikaji.


Rais Dkt. Samia pia aliwahimiza viongozi kuuenzi mchango wa Marehemu kwa kuimarisha mshikamano wa kitaifa na huduma bora kwa wananchi. 


Aidha, aliwapa pole familia, ndugu, wananchi wa Peramiho, Bunge na Taifa kwa ujumla, akiiomba Mwenyezi Mungu awape faraja, nguvu na amani, huku akiiombea roho ya Marehemu pumziko la amani ya milele.






Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.