RC CHALAMILA USO KWA USO NA WANAFUNZI WA CHUO CHA NIT-DSM.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amefanya ziara ya kutembelea Chuo cha Taifa cha usafirishaji na kuwataka wanafunzi wa vyuo kujiepusha na vitendo visivyoendana na malengo yao ya kielimu kwani Taaluma yao ni muhimu kwao, familia zao na Taifa kwa ujumla hivyo asitokee mtu akawatoa kwenye lengo lao la elimu
RC Chalamila akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara hiyo amesema vipo vishawishi vingi wanavyoweza kukutana navyo katika safari yao ya kutafuta elimu hivyo ni muhimu kwao kuwa na (focus) au malengo na mipango ya kihakikisha wanatimiza kile kilichowapeleka vyuoni na hatimaye kuwa na maisha ya ndoto zao
Aidha RC Chalamila amesema kwa sasa Serikali ya awamu ya sita imefanya maboresho makubwa kwenye vyuo ikiwemo miundombinu na upatikanaji wa rasilimali muhimu kama vile fedha za kujikimu tofauti na miaka ya nyuma hivyo amewasisitiza kujielekeza kwenye malengo yao na kuepuka vishawishi hasa vilivyopo mitandaoni kwani vinaweza kuwapotezea lengo na kuharibu mustakbali wa maisha yao pia kushindwa hata kusaidia wazazi wao
Sanjari na hilo RC Chalamila amewatoa shaka juu ya fikra za ajira baada ya masomo yao ambapo amewasisitiza kupata viwango vya juu vya ufaulu kwa kuwa ajira za Serikali na Taasisi binafsi za ndani na hata nje ya nchi zinahitaji wahitimu wenye ufaulu wa juu na wenye ubunifu hivyo asitokee mtu akawatoa kwenye lengo na kuwakosesha sifa
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha NIT Prof Prosper Mgaya na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Wakili Albert Msando wamezungumzia namna ambavyo Serikali imeendelea kuimarisha mazingira ya upatikanaji wa elimu na kuwasisitiza wanafunzi kujielekeza kwenye elimu na,kuacha serikali kushughulikia changamoto zao zinazowakabili
Naye Rais wa Serikali ya wanafumzi wa chuo hicho cha Taifa cha usafirishaji NIT Bw Wilium Mvungi ameishukuru Serikali kwa namna ambavyo inaendelea kuboresha mazingira ya chuo hicho ambacho kwa sasa kimefisha miaka 50.



Comments
Post a Comment