MAONESHO YA 12 YA BIASHARA YAZINDULIWA ZANZIBAR, TMA YASHIRIKI KIKAMILIFU.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amezindua rasmi Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar (ZITF) katika viwanja vya Nyamanzi Januari 7, 2026. Ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji na wafanyabiashara, huku akisisitiza umuhimu wa sekta binafsi katika kufanikisha maendeleo endelevu ya taifa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Hemed alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuboresha mazingira rafiki kwa wawekezaji na wafanyabiashara, akisisitiza kuwa sekta binafsi ni nguzo muhimu katika kufanikisha maendeleo endelevu ya taifa.
Katika maonesho hayo, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeshiriki kikamilifu, ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa TMA Ofisi ya Zanzibar, Masoud Makame Faki.
Akiwahutubia wananchi, Faki aliwataka kutembelea banda la TMA ili kupata elimu kuhusu sayansi ya hali ya hewa, hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Alibainisha kuwa mabadiliko haya yamekuwa yakisababisha athari katika sekta mbalimbali za uchumi na kijamii.
Aidha, alisisitiza kuwa matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa ni muhimu katika kuongeza tija na kuimarisha uchumi kwenye sekta kama kilimo, uvuvi, viwanda, nishati, ujenzi na mawasiliano.


Comments
Post a Comment