RAIS DKT. MWINYI AZINDUA RASMI VIWANJA VYA GOMBANI PEMBA.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 13 Januari 2026, amevizindua rasmi Viwanja vya Michezo vya Gombani vilivyopo Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.


Uzinduzi wa Viwanja vya Michezo vya Gombani umefuatiwa na Mchezo wa Fainali ya NMB Mapinduzi Cup 2026 uliozikutanisha klabu kongwe za soka nchini, Azam FC na Yanga SC, mchezo uliovutia maelfu ya mashabiki wa soka kutoka ndani na nje ya Zanzibar.


Uwanja wa Gombani Umefanyiwa Ukarabati Mkubwa  na Kampuni ya  Reform Sports pamoja na Ujenzi wa Uwanja wa Wilaya  ya Chakechake  na kiwanja  cha Michezo mengine  ikiwemo Mpira wa Mikono , Mpira wa Wavu na Mpira wa Kikapu  pembezoni mwa Uwanja wa  Mkubwa wa Gombani.


Uzinduzi huo  ni Miongoni mwa Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.






Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.