TMA YATOA ANGALIZO: UPEPO MKALI NA MAWIMBI MAKUBWA PWANI YA BAHARI YA HINDI.

 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la siku mbili kuanzia Januari 8 hadi 9, 2026, kuhusu uwepo wa upepo mkali unaoweza kufikia hadi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yenye urefu wa hadi mita mbili katika ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi.


Kwa mujibu wa TMA, maeneo yatakayoguswa ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikiwemo visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, huku baadhi ya maeneo ya Lindi na Mtwara yakitarajiwa kupata mawimbi makubwa katika kipindi hicho.


Hata huvyo Mamlaka hiyo imetahadharisha  hali hiyo inaweza kuathiri shughuli za uvuvi na usafiri wa baharini, hasa kwa vyombo vidogo, na hivyo imewataka wavuvi na wasafiri kupanga safari zao kwa kuzingatia tahadhari hiyo na kufuatilia taarifa zinazotolewa mara kwa mara.







Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.