DKT. MWIGULU KUMWAKILISHA RAIS SAMIA CONGO BRAZAVILLE.


Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ameondoka nchini leo, Jumatatu Mei 25, 2026, kuelekea Brazzaville, Jamhuri ya Kongo, kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).


Mkutano huo utaanza Mei 26 hadi 27, 2026 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kintele, ambapo unatarajiwa kuwakutanisha takribani washiriki 3,000 kutoka mataifa mbalimbali.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mkutano huo ni jukwaa muhimu la kimkakati linalowakutanisha Mawaziri wa Fedha, Magavana wa Benki Kuu, watunga sera, taasisi za kifedha, sekta binafsi, wawekezaji na washirika wa maendeleo kujadili masuala ya ukuaji wa uchumi barani Afrika.


Aidha, mkutano huo unalenga kuimarisha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya Afrika pamoja na kuongeza uwezo wa bara hilo kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kifedha duniani.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.