RC CHALAMILA ATEMBELEA TFF MAKAO MAKUU-DSM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametembelea shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF na kulipongeza shirikisho hilo kwa kuiwezesha timu ya vijana chini ya miaka 17 kufuzu kuingia katika mashindano ya kombe la Dunia kwa vijana chini ya miala 17 lakini pia kufanya vizuri ligi kuu ya Tanzania Bara NBC Premier league kuwa ni moja ya ligi bora 10 Barani Afrika
Akizungumza Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kutembelea makao makuu ya shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF yaliopo Ilala Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amesema shirikisho hilo limeonesha weledi na uzalengo mkubwa kuinua kiwango cha soka nchini Tanzania kwani timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 imeendelea kufanya vyema na kufuzu kuingia kombe la Dunia
RC Chalamila amesema kuwa mafanikio hayo ikiwemo kufanya vizuri kwa timu za Tanzania zinazoshiriki mashindano ya kimataifa zimepewa nguvu na uongozi imara ulioamua kuwekeza na kuwezesha vijana kupitia michezo chini Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hadi kupelekea Tanzania kupata heshima ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON mwaka 2027
Akizungumzia maandalizi ya mashindano ya AFCON ya mwaka 2027 RC Chalamila amesema Rais Dkt Samia ameendelea kuboresha miundombinu ya barabara, Umeme, Maji pamoja na ulinzi na usalama sanjari na mkakati wa kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa Smart City ili matukio yote yaweze kuratibiwa kidigitali ili kuweza kupokea wageni hivyo ameitaka TFF kuweka mazingira ya timu ya Taifa ya Tanzania kufanya vyema kwenye mashindano hayo
Aidha Chalamila amesema amepokea changamoto za miundombinu ya uwanja wa mpira wa karume uliopo makao makuu ya TFF pamoja na ofisi hiyo kwa ujumla ambapo amesema anakwenda kuitisha kikao cha Halmashairi zote ili kushughulikia suala hilo kwa kishirikiana na wadau binafsi ili kuwa mazingira bora ya kuendeleza soka nchini.
Akihitimisha mazungumzo yake na vyombo vya habari Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amewatoa shaka wakazi wa Jiji hilo juu ya ulinzi na usalama wa Mkoa huo kwani Serikali inasimamia usalama wa raia na mali zao bila kujali itikadi za vyama, dini ama kabila huku akzungumzia tukio la mchina ambae anatajwa kuuawa na wafanyakazi wake.
Kwa upande wake Rais wa TFF Walecy Karia ameeleza namna shirikisho linavyosimamia watoto kwenye michezo kuanzia umri wa miaka 10 hadi 17 huku akieleza mikakati ya ujenzi wa uwanja wa karume kwa mfumo mpya unaoruhusu uwepo wa michezo na shughuli za biashara.
Pia amewataka wanahabari kulisaidia shirikisho hilo kuondoa usimba na uyanga pale kunapokuwa na michuano ya kimataifa inayohitaji wachezaji kutoka timu hizo kwenda timu ya Taifa




Comments
Post a Comment