TET, Montessori Community Tanzania zasaini makubaliano ya kuboresha elimu nchini


Na Mwandishi Wetu

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Shirika la Montessori Community of Tanzania zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano wenye lengo la kukuza ubora wa elimu nchini kupitia maboresho ya mitaala na uboreshaji wa stadi za wanafunzi.

Hafla hiyo fupi imefanyika Mei 25, 2026 katika ofisi za TET makao makuu jijini Dar es Salaam, ikihudhuriwa na viongozi wa taasisi hizo pamoja na wajumbe wa menejimenti.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Aneth Komba amesema taasisi hiyo iko tayari kushirikiana na Montessori Community of Tanzania ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora inayokidhi stadi za karne ya 21, kufuatia maboresho ya mtaala.

“Tumejipanga kuhakikisha mtaala ulioboreshwa unaleta matokeo chanya kwa wanafunzi na kuwajengea uwezo unaohitajika katika dunia ya sasa,” amesema Dkt. Komba.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Montessori Community of Tanzania, Bi. Sarah Kiteleja, ameishukuru Serikali kupitia TET kwa kukubali ushirikiano huo, akisema utaimarisha zaidi malezi, makuzi na mafunzo kwa wanafunzi.

Amesema ushirikiano huo utasaidia kuendana na mabadiliko ya mtaala mpya unaolenga kumjenga mwanafunzi kwa ujuzi na ubunifu zaidi.






Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.