ANGALIZO LA UPEPO MKALI KWA UKANDA WA PWANI.



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la upepo mkali unaotarajiwa kufikia kasi ya kilomita 40 kwa saa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi kuanzia Juni 14 hadi 16, 2026.


Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikiwemo visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.


Kwa mujibu wa TMA, upepo huo unaweza kuathiri baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafiri wa baharini. Kiwango cha athari kinatarajiwa kuwa cha wastani.


Wananchi, hususan wavuvi na watumiaji wa vyombo vya usafiri wa majini, wanashauriwa kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa na kuchukua tahadhari stahiki ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.